Michoro ya Kitanzania

 

Lucas Tenga ni mmoja wa wasanii 'waliojificha' nchini Tanzania, lakini ambaye kazi zake zinavutia watu wengi, hususan kutoka nje ya nchi.

Ukimtembelea kwenye 'ofisi' yake Mjini Moshi jirani na soko kuu, utamkuta ni kijana mtaratibu asiye na makuu. Karibu maduka yote ya Kilimanjaro yauzayo sanaa za asili, yamejaa bidhaa zilizotengenezwa na Tenga.

Picha za hapa chini ni mfano tu wa kazi zake. Hakika anastahili sapoti ya kila mmoja, hususan mashirika na wote wanaohamasisha sanaa.

Waweza kumtumia ujumbe kupitia anuani hii:

 

Lucas Tenga
P.o. box 8844
Moshi,
Tanzania, East Africa.

 

  Ngoma ya Wamasai
 
  • Wamasai, wakicheza ngoma.
   
  Tingatinga
 
  • Mchoro mtindo wa 'Tingatinga'
   
  Kupanda Mlima Kilimanjaro, Tanzania
 
  • Mtalii akipanda Mlima Kilimanjaro, mlima ulio
    nchini Tanzania
   

Haki zote zimehifadhiwa.

(C) 2000 Chumvi Mtembezi
Email: chumvi.mtembezi@usa.net
http://chumvi.tripod.com