Watu wengi wamekuwa wakiuliza masuali mengi kuhusu webusaiti hii. Yafuatayo ni baadhi ya maswali hayo.


Maswali Yaulizwayo Sana (MAS)

  1. Webusaiti yako ni 'bomu', unapata faida gani kupoteza muda kuijenga ... ?
  2. Kweli wewe umeenda shule ... ?
  3. Hadithi zilizoko humu ni wewe ulizitunga ... ?
  4. Hivi Chumvi Mtembezi ni nani ... ?
  5. N'shakufahamu ... wewe unaitwa Shomvi Mukebezi!
  6. Ninaweza kutumia wazimu ulioko humu kufundishia ... ?

Webusaiti yako ni 'bomu', unapata faida gani kupoteza muda kuijenga... ?

Furaha yangu ni kuona wapo watu wanaosoma 'wehu' uliomo humu, na kukikuza Kiswahili.

Rudi Mwanzo

Kweli wewe umeenda shule ... ?

Hapana! Shule niliyoenda inatosha kujaribu kufuta ujinga.

Rudi mwanzo

Hadithi zilizoko humu ni wewe ulizitunga ... ?

Hadithi hizo zimetungwa na 'Mwandishi Mualikwa'.

Rudi mwanzo

Hivi Chumvi Mtembezi ni nani ... ?

Hilo ni swali zuri... Ni kwa sababu yaliyomo humu yametiwa 'chumvi' na halafu 'yanatembea' mbali mpaka wewe ukaweza kuyafahamu.

Rudi mwanzo

N'shakufahamu! Wewe unaitwa Shomvi Mukebezi ... !

'Kula jiwe'!

Rudi mwanzo

Ninaweza kutumia 'wazimu' ulioko humu kufundishia ... ?

Sina mbungi! Wewe nitumie imeili tu ikiwa utataka kutengeneza chapisho.

Rudi Mwanzo

Chumvi Mtembezi
Hakimiliki © 2000 Chumvi Mtembezi. Haki zote zimehifadhiwa.
Imerejewa: Juni 30, 2000..